The House of Favourite Newspapers

Breaking: Jeshi Laipindua Serikali ya Bongo

KUNDI la wanajeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

 

Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu, Libreville. Shirika la habari la AFP inasema milio ya risasi imesikika jijini humo.

 

Tangazo kutoka  kundi la vijana wa umri wa makamo limetolwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanajeshihao wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.

 

Walichukua udhibiti wa kituo hicho cha redio majira ya saa kumi alfajiri (saa kumi na mbili alfajiri Afrika Mashariki).

 

Wanajeshi hao wamesema wamechukua hatua hiyo “kurejesha demokrasia” na wametangaza kwamba wanataka kuunda ‘Baraza la Taifa la Ufufuzi/Ukombozi’.

 

Wamekosoa hotuba ya Mwaka Mpya iliyotolewa na Rais Bongo mnamo 31 Desemba, na wanasema kwenye hotuba hiyo mawazo yake yalionekana kutotiririka na sauti yake ilikuwa dhaifu.

 

Bw. Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa na baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia 24 Oktoba kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi nchini humo.

 

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.

 

Rais Ali Bongo alichukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kutoka kwa baba yake, Omar Bongo, mwaka 2009, ambaye aliiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa zaidi ya miaka 40.

 

 

Alishinda uchaguzi wa marudio mwaka 2016, katika zoezi lililotawaliwa na ghasia na tuhuma za udanganyifu.

 

Katika uchaguzi huo, Bongo alipata ushindi kwa 49.8% ya kura na  Jean Ping akapata 48.2 % ya kura, kura zilizowatenganisha zikiwa 5,594.

 

Ping alisema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na “hakuna ajuaye” hasa nani alishinda.

 

Kabla ya kuingia katika siasa, Ping aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

 

Comments are closed.