BREAKING: Joshua Nassari Ahamia CCM Arusha – (Pichaz +Video)

ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Akizungumza katika mkutano wa kupokelewa na viongozi wa CCM Mkoa wa Arusha,  Nassari amesema kuwa amejiunga na chama hicho ili kujiweka katika upande mmoja na wale wanaoitakia nchi hii maendeleo.

 

Nassari ameongeza kuwa serikali ya Rais John Magufuli imefanya mambo mengi ambayo amekuwa akiyapigania kama vile kuboresha elimu, huduma za afya na ujenzi wa miundombinu  na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati, hivyo hakuna sababu yoyote ya kumpinga.

“Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana nchini, tuliyoyapigania kwa Miaka Mingi, Nimpinge Ili Iweje? ” amesema Nassari.

 

Nassari alivuliwa ubunge wake Machi 2019 kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya bunge mfululizo bila ruhusa, kitendo ambacho ni kinyume na sheria

Alichokisema Joshua Nassari baada ya kujiunga na CCM

“Wengine wanasema Nassari ubunge, niwaambie sijatangaza nia mahali popote, na sijaja CCM kutangaza nia, nimetafakari na pia jamii, wazee wa Meru na marafiki waliofanya nikawa mbunge mdogo kuliko wote nchi hii wameniambia. Naona CCM huku kunafaa.

“Haikuwa kazi rahisi kufanya haya maamuzi ya kuja CCM. Yote mnayotaka kuyasikia na kuyaona kutoka kwangu mtayasikia na kuyaona hata kama siyo leo. Sababu kubwa iliyonileta CCM ni kwa kuwa naipenda Nchi yangu.

“Ukiongea habari ya ndege wapingaji wanasema nani anapanda? Mbona wakati wa Mwalimu Nyerere hamkusema Mwalimu unatupa ndege hatuna hela ya kupanda? Leo tuna ndege kumi na moja. Ile moja ni USD Mil 31. Nimeingia bungeni hatuna hata ndege, unaachaje kumuunga mkono JPM?

“Nimeamua kuiweka nchi yangu mbele. Najua wapo watakaonitukana, watakaosema hili na lile kisa mimi kuhamia CCM lakini sitojali. Nawashukuru watu wa Meru kwa kuniamini kwa mihula miwili mfululizo nikiwa mbunge mdogo kuliko wote Tanzania.

 

“Watanzania wanaokwazwa kwa kuona nimeingia CCM ambao walitamani kuendelea kuniona upinzani naomba mnisamehe. Siwezi kuendelea kuwa mnafiki, roho yangu imekataa. Sijatangaza nia na huenda nisichukue fomu, mkisema tunataka tukupe semeni hayo baadaye.

 

“Mengi tutayazungumza huko mbele. Nilichagua kuingia kwenye siasa ili kuijenga nchi ndiyo maana nilichimba visima, nilinunua vitanda hospitali. Sasa yote ambayo nilikuwa napigania JPM ameyafanya nikimpinga nitaonekana sina akili.

“Siku zote nafanya siasa za kiungwana. Nimeshawaandikia barua Chadema na kiukweli naishukuru Chadema ilinichukua nikiwa mdogo wakanisikiliza wakaona kuna potential ndani yangu. Nawashukuru kwa kunilea nitakuwa mjinga kama sitoikumbuka historia.

“Kuna tabia ipo maana mimi ni mfugaji kule Meru, kondoo mpya akiingia zizini wenziye wanaanza kumnusanusa kwamba huyu siyo wa hapa. Watu wa CCM msininusenuse, mimi mwenzenu. Nimekuja kujenga nchi.”

 Tecno


Toa comment