JPM Awapa Ofa Wataalamu wa Moyo Kutoka Israel na Marekani – Video

Rais Dkt. John Pombe Magufuli anakutana na timu ya wataalamu wa matibabu ya moyo kutoka nchini Israel na Marekani, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo asubuhi (Novemba 08, 2018) wataalamu hawa wanashirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

 

Akizungumza na wataalam hao Ikulu jijini Dar es salaam, Rais amesema“Mtu mwenye moyo safi maisha, yake kazi yake inakua kuokoa maisha ya wengine, nawashukuru sana madaktari kutoka Israel, nimeandika barua ambayo mtampelekea Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuonyesha appreciation yangu, najua hii barua itamfikia ili kuonesha kazi nzuri mliofanya.

 

“Tanzania itaendelea kushirikiana na Israel, itashirikiana na Marekani, ndiyo maana katika awamu hii niliamua kufungua Ubalozi wa Israel kwa makusudi, urafiki kati ya Tanzania na Isarel utaendelea kudumu.

“Niwaombe Madaktari na Wataalamu kutoka Israel mkija msije tu kwa masuala ya Udaktari siku nyingine mnaweza mkaja kwa masuala ya kufurahi, mnaenda Serengeti National Park, Ngorongoro na maeneo mengine ambayo ni ya kuvutia. Naomba mtenge siku mbili hata tatu tuwapeleke Serengeti Nationa Park au Ngorongoro mkakae hamtalipa chochote, ofa itatolewa na Serikali lakini mkiona haiwezekani kwa sasa ofa itabaki palepale mnaweza mkapanga ratiba nyingine mkaja.

 

“Tenda ya kusambaza madawa katika nchi za SADC tumepewa Tanzania. Ndugu zangu mliokuja kushughulikia watoto 51 mtakaporudi Israel msiisahau Tanzania, mjue tunahitaji misaada yenu, kama kuna ndugu zetu Israel wanaweza kutoa donation za aina yoyote katika Hospitali zetu itakuwa vizuri, mjue Tanzania inawahitaji,” amesema Rais Magufuli.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILI HAPA

Toa comment