The House of Favourite Newspapers

BREAKING: JPM Amng’oa KAIRUKI Wizara ya Madini, Biteko Ala Shavu!

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, akitangaza mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri  na uteuzi wa viongozi wapya kadhaa uliofanywa na Rais  John  Magufuli, leo Jumanne, Januari 8, 2019.

RAIS  John Magufuli leo, Januari 8, 2019, amefanya uteuzi wa viongozi na mabadiliko kidogo ya ofisi ambayo yalitangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi, kama ifuatavyo:

 

Amekihamisha kituo cha uwekezaji nchini (TIC) kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kukipeleka Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuongeza msukumo katika masuala ya uwekezaji.  Vilevile amemteua Angela Kairuki kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu/Uwekezaji, ikiwa ni wizara mpya

 

Rais pia amemteua Mhe. Dotto Biteko kuwa Waziri Wizara ya Madini ambapo kabla ya hapo alikuwa ni naibu katika wizara hiyo ambapo  Stanslaus Nyongo ataendelea kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Madini pekee, ambapo kabla ya hapo manaibu waziri walikuwa wawili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu /Uwekezaji, Angela Kairuki.

Kwa upande wa makatibu wakuu, Rais ameteua makatibu wakuu wanne ambapo Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ni Joseph Nyamhanga ambaye amechukua nafasi ya Yombe; Katibu Mkuu Wizara ya Afya amekuwa Zainab Chaula ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Tamisemi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi ni  Elius Mwakalinga ambapo katika Sera na Uwekezaji ni Dorothy Mwaluko.  Pia Naibu Katibu Mkuu Tamisemi  ni Dorothy Gwajima atakayeshughulikia Afya

Naibu Katibu Mkuu Utumishi aliyeteuliwa ni Francis Michael aliyekuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika mabadiliko hayo, nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi imefutwa na katika mabadiliko hayo Dr. Mpoki Ulisubisya ameteuliwa kuwa balozi ambapo kituo chake kitatangazwa baadayee.

Kabla ya uteuzi Dr. Ulisubisya alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, na katika mwendelezo wa mabadiliko hayo, serikali imefungua ubalozi wa Tanzania nchini Cuba.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko.

Comments are closed.