RAIS wa Tanzania, John Magufuli, amemteua na kumuapisha Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuchukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa uteuzi wake umeanza leo.
Kabla ya uteuzi huo, Diwani aliyeapishwa Ikulu, Dar es Salaam leo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Akizungumza baada ya kumwapisha, Rais Magufuli amemtaka kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuweka mbele maslahi ya taifa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kapilimba atapangiwa kazi nyingine.
Athumani aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Septemba 6, 2018, nafasi aliyoitumikia kwa mwaka mmoja na siku sita. Kabla ya kwenda Takukuru alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) Kagera.
Nafasi alizoshika Kamishna Diwani Msuya tangu 2015:
⭕️2015: Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai
⭕️Mei 2015: Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)
⭕️Nov. 2016: Katibu Tawala Kagera
⭕️Sep. 2018: Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU
⭕️Sep. 2019: Mkurugenzi Mkuu TISS
Picha na Ikulu
Comments are closed.