The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MBUNGE KATANI HAJAJIUZULU

MBUNGE wa Jimbo la Tandahimba, Mtwara kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Katani Ahmadi Katani, hajajiuzulu Ubunge wa Tandahimba kama taarifa zilivyokuwa zikisambaa mitandaoni.

 

Mbunge huyo yupo bungeni jioni hii ya leo Alhamisi, Novemba 15, 2018, na amepata fursa ya kuchangia mjadala na kuvitaka vyombo vya habari kumuomba radhi kwa kuandika habari kuwa amejiuzulu.

 

Taarifa potofu zilizosambaa leo mchana zilieleza kuwa Katanni amejiuzulu ubunge na nafasi zake zote ndani ya CUF kwa madai ya kuwepo migogoro isiyokwisha ndani ya chama chake inayoathiri utendaji kazi wake.

Aidha, aliyekuwa Mbunge wa TEMEKE (CUF), Abdallah Mtolea amejiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya CUF akidai kumekuwa na migogoro mingi ndani ya chama chake. Mtolea ametoa tamko hilo leo Nov 15, ndani ya Bunge na kusema bado anatamani kuwatumikia wananchi wa TEMEKE.

 

Dakika chache baada ya Abdallah Mtolea kujivua ubunge wa Jimbo la Temeke akidai kuchoshwa na migogoro ndani ya chama chake cha CUF, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Magdalena Sakaya amesema mbunge huyo alikuwa ni moja ya chanzo cha migogoro na kujiondoa kwakwe ni ‘kujiwahi’.

Comments are closed.