Breaking: Kenya Yafunga Mipaka Yake Tanzania na Somalia

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kufungwa kwa mipaka yake na Mataifa ya Tanzania na Somalia kuanzia usiku wa  kwa siku 30 zijazo

Rais Kenyatta amesema kuwa ni madereva wa magari ya kubeba mizigo pekee ambao wataruhisiwa kuingia nchini Kenya baada ya kupimwa COVID19 na kupatikana kuwa hawana.

Amesema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya madereva wa malori ya kubeba mizigo 78 raia wa kigeni kunyimwa kibali cha kuingia nchini Kenya baada ya kukutwa na virusi hivyo.

Kenya aidha imeongeza muda wa marufuku ya kutoka nje kwa siku 21 zijazo hadi Juni 6, 2020

Kufikia sasa idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 830 baada wagonjwa wapya 49 kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo.Waliofariki kutokana na corona ni watu 50 baada ya wengine watano kufa.Rais Kenyata pia ametangaza kuwa wagonjwa 17 wametolewa hospitalini walipokuwa wakipata matibabu.
Toa comment