The House of Favourite Newspapers

Lema Akamatwa Hai Kwa Agizo La Ole Sabaya – Video

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai (Chadema), Helga Mchomvu, leo Alhamisi Novemba 14,2019 wamekamatwa na polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya.

Akizungumza na GlobaTV Online, Sabaya amethibitisha kukamatwa kwa Lema na Mchomvu.

 

Sabaya amedai kiini cha kuagiza viongozi hao wakamatwe ni kutokana na kile alichokiita kuendeleza njama zao za kuvuruga amani katika wilaya hiyo na kusababisha taharuki kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

 

“Kitendo cha mbunge Lema kutoka Arusha na kuja hapa Hai na kufanya vikao vya siri ni sawa na kuvuka mstari mwekundu na hili sisi kama Serikali hatuwezi kulivumilia. Namtaka Lema ajisalimishe mwenyewe polisi,” amesisitiza Sabaya.

 

Comments are closed.