BREAKING: LORI LA MAFUTA LALIPUKA, LAUA WATU 55 MORO (PICHA +VIDEO)

Wananchi wakiendelea kufanya uhokoaji eneo la tukio baada ya lori la mafuta kulipuka leo mkoani Morogoro.

LORI la mafuta limelipuka asubuhi hii Agosti 10, 2019, maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro na kuua watu zaidi ya  57 wakati wakijaribu kuchota mafuta baada ya gari la kubebea mafuta kupata ajali mjini Morogoro.  Inasemekana pia  watu 55 wamepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili kutokana na moto huo.

Mashuhuda wanadai moto ulianza baada ya mtu mmoja kuchomoa betri  ya gari na kusababisha cheche zilizoibua moto huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa,  amesema karibu watu zaidi ya 57 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi ya leo.

Lori hilo lilikuwa linatoka jijini Dar es Salaam ambapo lilipinduka na kuangukia upande wa kulia wa barabara  ya kuelekea Iringa na mafuta  yakaanza kumwagika  na ndipo watu waliokuwa jirani wakiwemo waendesha bodaboda na watu wengine,  walianza kuchota mafuta hayo na ghafla ukatokea mlipuko mkubwa uliozua moto huo na kusababisha maafa hayo.

Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.

Bodaboda zikiwa zimeteketea kwa moto baada ya lori kulipuka.

 

Stori na Dustan Shekidele, Morogoro | GPL


Loading...

Toa comment