Kesi ya Chadema Yaahirishwa tena, Mbowe arudishwa Rumande

 

 

Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee kuendelea na majukumu yake ya ubunge nje ya nchi yaliyomfanya ashindwe kufika mahakamani leo Desemba 6, 2018 kwa ajili ya kesi ya jinai inayomkabili.

 

Mdee na viongozi wakuu wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, wanakabiliwa na mashtaka 13 ya uchochezi, uasi na kuhamasisha wafuasi wao kutenda makosa, hakuweza kufika mahakamani wakati kesi yao ilipotajwa leo.

 

Akitoa uamuzi Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbald Mashauri,  amesema kwa kuwa alipokea nakala ya barua ya Bunge ikimwombea ruhusa Mdee anakubali aendelee na shughuli zake hizo.

Kuhusu Heche amesema pia anamruhusu aendelee na ruhusa yake ya kumuuguza mkewe ambayo alishampatia.

 

Hata hivyo amewataka wote wawepo tarehe kesi hiyo itakapotajwa, akiwa ameiahirisha hadi Desemba 21, 2018.

Mbali na Mdee Mdee, Heche na Mbowe, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu, Dkt. Vicent Mashinji; naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Wengine ni mweka hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

 

Toa comment