Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho, wamefutiwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar walipokuwa wameripoti kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa na Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Kanda (ZCO) na kupelekwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashitaka yanayowakabili.
Mbowe na viongozi wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Vincent Mashinji; Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu; Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama, Peter Msigwa na Ester Matiko, wamefikishwa Mahakamani hapo kwa tuhuma za kuendesha maandamano kinyume na taratibu.
Maandamano yanayodaiwa kuendeshwa na viongozi hao ni yale yaliyofanyika Februari 16, mwaka huu na kusababisha polisi kuwatawanya waandamanaji na kupelekea kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwilini maeneo ya Kinondoni jijini Dar.
BREAKING NEWS: MBOWE, MASHINJI, MNYIKA WAPANDISHWA MAHAKAMANI (VIDEO)
Comments are closed.