The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Makonda Asema Wabunge Ubungo, Kibamba Waomba Kusajiliwa CCM – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  amesema amepokea maombi mbalimbali ya madiwani na wabunge wawili — majimbo ya Ubungo na Kibamba —  wa chama cha upinzani wanoataka kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wabunge wa sasa wa majimbo hayo ni kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  ambao ni Saed Kubenea (Ubungo) na John Mnyika (Kibamba).
 
Makonda ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa uwekaji  jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Selander na barabara unganishi jijini Dar es Salaam ambapo alisema miongoni mwa watu wanaotaka kujiunga na CCM ni pamoja na madiwani kutoka upinzani.
 
“Kilichotokea Temeke ni toba, Ukonga ni toba, kilichotokea Kinondoni ni toba… huku kwenye kata kuna toba nyingi sana zinafanyika, kwa waungwana walipoingia wamegundua kile chama hakina ilani inayotekelezeka.
“Wengi wameniomba kujiunga CCM, wapo madiwani na wabunge wa Ubungo na Kibamba… walikuwa wanasema kama deadline (tarehe ya mwisho) imeshatoka itakuwaje? Nikawaambia ngoja tuangalie kama kuna usajili wa dirishani Katibu Mkuu akiruhusu tuone itakuwaje.”

Comments are closed.