#BREAKING! MTANDAO wa Madawa ya Kulevya WANASWA – Video

JESHI  la polisi nchini,  kupitia kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,  linawashikilia watu saba ambao wanadaiwa wapo kwenye mtandao wa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

 

Akizungumza na waandishi wa habari,  Kamishna Msaidizi wa Polis,i ACP Salim Hassan, amesema  watu hao wamekamatwa kutokana na oparesheni maalum na watafikishwa mahakamani ushahidi ukikamilika.

 

Aidha amesema jeshi lake kitengo cha kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na wakuu wa upelelezi wa mkoa na kamati za ulinzi na usalama, limejipanga kuhakikisha suala la usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya linatokomezwa.

 

Hata hivyo,  jeshi hilo limetoa rai kwa  wote wanaoendelea na biashara hii haramu waache mara moja kwani oparesheni hii ni endelevu.

 

TAZAMA TUKIO HILO


Loading...

Toa comment