The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Mtatiro Ajiondoa CUF, Ajiunga CCM -VIDEO

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Julius Mtatiro.

Aliyekuwa Kada wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya chama hicho, Julius Mtatiro amejivua uanachama wa chama hicho nakujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akisema kuwa huu ni wakati wake wakwenda kutumia vipaji vyake kikamilifu pia kuwa balozi mkubwa wa Rais Magufuli Ndani na nje ya Nchi.

Julius Mtatiro akiongea na wanahabari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa jukwaa alilokuwa analisimamia katika siasa kwa miaka kumi limeshindwa kumpa nafasi yakuifanyie nchi yake maendeleo.

 

Katika hatua nyingine baada ya kutangaza nia hiyo Mtatiro ametoa ahadi yakuwatumikia watanzania pamoja na kupambana na umasikini nakuongeza uamuzi alioufanya sio kwaajili yakutafuta cheo.

(PICHA: DENIS MTIMA | GPL)

Comments are closed.