The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MUNA LOVE Afunguka Yote Kifo cha Patrick – Video

Ikiwa zimepita wiki mbili tangu mtoto wa Muigizaji Muna Love anayeitwa Patrick azikwe katika makaburi ya Kinondoni na kifo chake kuibua gumzo kuhusiana na nani ni baba mzazi wa mtoto huyo ambapo alihusishwa Mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson na Peter Zakaria Komu, hatimaye muigizaji huyo leo ameamua kuzungumza na waandishi wa habari na kufafanua sintofahamu zote zilizotokea wakati wa mazishi ya mwanae.

 

“Mwanzoni Patrick alikuwa anaumwa mguu, nilimpeleka Hospitali ya Aga Khan wakasema hana tatizo, nikampeleka Muhimbili ikaonekana kwenye nyonga palikuwa pamesagika, wakamuwekea vyuma. Baadaye ikaonekana vyma vinamla wakamfanyia upasuaji kuviondoa na kukutwa usaha. Patrick aliniambia mama ukitaka nipone basi uokoke, nilijua ni maneno yake tu sababu ya ugonjwa lakini baadaye hali ilibadilika, nilienda Muhimbili Kanisani kwa watu wanaosalisha kama kuna musiba, nikamkuta mtumishi nikamwambia, alinisalisha sala ya toba, nikarudi.

 

“Kuna madini ya kuagiza kwa ajili ya kuweka kwenye huo mguu, ambayo gaharama yake ni Tsh. 50m. Wakasema kwa msaada madini yale tungeuziwa kwa Tsh. 25M, nikamwambia dakatari ngoja nijipange sinapesa. Baadaye daktari akasema Patrick anatakiwa afanyiwe upasuaji kesho. Patrick alisema “mama ninataka ukasaini nikafanyiwe upasuaji, nikiwa nafanyiwa upasuaji uniwekee nyimbo zangu. Madaktarai badala ya kutumia madini waliokuwa wamesema, walitumia mfupa mwingine wa kwenye mguu wake, walisema hatoweza kutembea mpaka amiezi 9.

 

“Patrick alizidiwa tena nikampeleka Aga Khan, walimpima hakuwa na ugonjwa wowote, wakatulaza, ikabidi apimwe kipimo kikubwa cha RMI, madaktari wakakuta ana uvimbe kwenye kichwa, na ndicho kilichokuwa kikimuumiza zaidi. Nikamuomba daktari aniandikie nikampime tena Aga Khan ya Kenya ili nijiridhishe kama kweli ana huo uvimbe au kama ana kansa. Nikaandikiwa barua na daktari akashauri mtoto asipande ndege kulingana na tataizo lake ni bora apande basi au private car.

 

“Tulifika Nairobi tukamkuta Joel Lwang alikuwa na event zake za dini,walitupokea na mwimbaji Mercy masika na mumewe David. Mercy aliniunganisha na daktari wa watoto aliyempima na kuniunganisha na daktari mwingine Bingwa wa watoto wa nchini Kenya anaitwa Dkt. Bole. Madaktari walisema ubongo wa Patrick hauwezi kuamshwa kwa dawa, badala yake utaamka wenyewe, tuliendelea na maombi pengine afya yake itarejea, lakini haikuwa rahisi. Mungu akaamua kumchukua na kumpumzisha,” alisema Muna.

Comments are closed.