The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Mwandishi Aliyetekwa Apatikana, Aeleza Mazito! – Video

MWANDISHI wa habari wa kujitegemea jijini Arusha, Lucas Muyovera amenusurika kuuawa kwa kipigo baada ya kutekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

 

Muyovera ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru akipatiwa matibabu inaelezwa hali yake ni mbaya baada ya watu wapatao watano kumteka Mei 14, 2018 majira ya saa 3  usiku katika eneo la Ngulelo jijini humo.

 

Kwa mujibu wa mwandishi huyo watu walimpakia kwenye gari yao na baadae kumpeleka katika mto ambao hajaufahamu na kuanza kumshambulia wakiwa wamemvua nguo zote na kumdhalilisha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limethibitisha tukio, hilo likidai bado wanafanya uchunguzi.

BREAKING: Mwandishi Aliyetekwa Apatikana, Aeleza Mazito! – Video

Comments are closed.