The House of Favourite Newspapers

Mchakato wa Sheria ya Vyama vya Siasa Kuanza Hivi Karibuni

Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano huo.

 

BARAZA la Vyama vya Siasa limesitisha mjadala wa mapendekezo ya marekebisho ya sheria mpya ya vyama vya siasa na kurudisha mchakato huo katika kamati ya sheria na utawala bora, kamati ya uongozi ya baraza hilo.

Sasa kamati hizo zinatakiwa kujadili marekebisho ya kanuni za usajili wa vyama vya siasa baada ya baraza hilo kushindwa kujadili.

 

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda (kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na kilichoendelea katika mkutano wao.

Akizungumza leo Januari 18, 2018 mwenyekiti wa baraza hilo, John Shibuda amesema mapendekezo hayo yanatakiwa kukamilika baada ya mwezi mmoja kabla ya kuitisha baraza maalum litakalopitia suala lililopaswa kufanywa leo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 38, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, Makamu Mwenyekiti wa CCM  Bara, Philip Mangula na  Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Dk Abdallah Juma  Saadala.

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

FUATILIA VIDEO YA TUKIO HILO

Comments are closed.