The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MWILI WA LEYLA WAWASILI NYUMBANI KWAO KALOLENI, ARUSHA

Mwili wa Mtanzania, Leyla Mtumwa anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu na mumewe, Kema Kasambula, mwezi uliopita jijini London nchini Uingereza umewasili nyumbani kwao Arusha jioni hii Jumatatu, Aprili 23, 2018 baada ya kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya shughuli ya mazishi.

Mwili wa Leyla ulikuwa ukishikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya kujiridhisha ndipo wakaukabidhi kwa familia.

Leyla anadaiwa kuuawa na mumewe huyo, usiku wa kuamkia Machi 30, mwaka huu jijini humo ambapo sasa jamaa huyo anakabiliwa na kesi ya mauaji.

Leyla ni mtoto wa Hidaya aliyeimbwa na Pepe Kalle kwenye wimbo wake wa Hidaya miaka ya 1990, mwenye makazi yake Kaloleni jijini Arusha ambako ndiko msiba ulipo. Taratibu za mazishi ya Leyla zitaanza kufanyika kesho Jumanne nyumbani kwao Arusha.

Comments are closed.