The House of Favourite Newspapers

Breaking: Ndege Ya Ethiopian Airlines Yaanguka

Ndege ya Kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka leo ilikuwa imebeba abiria 149 na wafanyakazi nane.

 

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Ethiopia imeanguka leo asubuhi majira ya saa mbili na dakika arobaini na nne kwa saa za Afrika Mashariki.

 

Msemaji wa shirika hilo ambaye hakutojwa jina lake  amethibitisha juu ya taarifa hiyo ambapo imetajwa ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini Nairobi nchini Kenya.

Waziri mkuu wa Ethiopia ameandika katika ukurasa wake wa Twitta leo Jumapili, 10.03.2019 ujumbe wa kutoa pole kwa familia za waliofiwa kufuatia ajali hiyo mbaya.Ingawa pia ujumbe huo haukutowa maelezo zaidi.Ujumbe umesema-

”Ofisi ya waziri mkuu kwa niaba ya serikali na wananchi wa Ethiopia tungependa kutowa pole zetu kwa familia zilizopoiteza wapendwa wao waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikielekea Nairobi Kenya asubuhi ya leo”

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea jijini Adis Ababa.

Comments are closed.