The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Abdul Nondo Arudishwa Iringa, Apandishwa Kizimbani

Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi, Abdul Nondo amerudishwa mkoani Iringa na kufikishwa Mahakama ya Wilaya. Awali Nondo alitolewa Iringa baada ya mahojihano na Polisi na kupelekwa Dar kwa Mkurugenzi wa Upelelezi makosa ya Jinai kwa mahojiano.

 

Kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, amesema dhamana ya Nondo itatazamwa Jumatatu ijayo Machi 26, baada ya hakimu kuomba kusoma sheria inasemaje juu ya kuzuiwa dhamana kwake.

 

Imeelezwa kuwa, Nondo amesomewa mashtaka kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo Mitandaoni na kosa la pili ni kudanganya kuwa alitekwa. Shauri limeahirishwa na mtuhumiwa amepelekwa rumande.

 

Rais Magufuli Akiwaapisha Mabalozi Wapya Ikulu (Video)

Comments are closed.