Breaking News: Amber Rutty Aachiwa Huru Leo

MSANII Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ ameachiwa huru leo Januari 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar baaada ya kulipa faini ya shilingi milioni 3 za Kitanzania baada ya kusota gerezani miezi kadhaa.

 

Septemba 25, mwaka jana, Amber Rutty na mumewe, Said Bakary walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shilingi milioni tatu kila mmoja baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu likiwemo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha zisizokuwa na maadili.

Kwa mujibu wa vyanzo vya huakika, Amber Rutty amefanikiwa kutoka jela katika Gereza la Segerea baada ya baadhi ya wasanii kuchanga kiasi cha cha shilingi milioni tatu kama faini aliyotakiwa kulipa katika Mahakama ya Kisutu.

Baada ya Amber Rutty kutoka jela sasa kazi imebaki kwa mumewe, Said ambapo mwanamama huyo atakuwa na jukumu la kukusanya michango ili kumlipia faini ya shilingi milioni tatu naye atoke jela.

STORI NA IMELDA MTEMA | GPL

Toa comment