The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Basi la Saratoga Lateketea kwa Moto

Basi la Kampuni ya Saratoga lililokuwa likitoka Kigoma kuelekea Sumbawanga limewaka moto na kuteketea katika Kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana bado.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno amesema jeshi lake linachunguza chanzo cha moto huo.

Bado haijafahamika iwapo kuna vifo au majeruhi kutokana na ajali hiyo mbaya.

Updates:

Eneo la tukio, baada ya basi mali la Saratoga lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Sumbawanga kuteketeka kwa moto katika Kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma.

Abiria wote 60 waliokuwa ndani ya basi hilo wamepona na baadhi ya mizigo imeokolewa.

Endelea kufuatilia mitandao ya Global Publishers na Global TV Online kwa taarifa zaidi.

Comments are closed.