The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Boban Asaini Yanga Miezi Sita

 

Kiungo wa kikosi cha African Lyon na mchezaji wa zamani wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ leo  amesaini mkataba wa miezi sita na Yanga.

 

Boban amejiunga na Yanga baada ya kuwa na msimu mzuri katika kikosi cha African Lyon akiwa ameifungia mabao mawili katika Ligi Kuu.

Awali kulikuwa na taarifa kwamba Boban alikuwa mbioni kujiunga na Kagera Sugar, lakini dakika za mwisho aliamua kuwapiga chenga mabosi wa Kaitaba na kumwaga wino Jangwani ili kuungana na swahiba wake, Kelvin Yondani.

Kiungo huyo aliyewahi kuzichezea Simba, Mbeya City, Friends Rangers na IF Gefle ya Sweden amependekezwa na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera.

Comments are closed.