The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Everton Wawasili Dar, Wayne Rooney Yumo

0

 

KLABU ya Everton ya Uingereza tayari imewasili katika ardhi ya Tanzania tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kesho dhidi ya Gor Mahia ya nchini  Kenya, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Everton wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar.

 

Wakali hao wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi na kupokelewa na uongozi wa wadhamini wao, SportPesa ambao ndio wamewaleta hapa nchini.

 

Wayne Rooney na wachezaji wenzake wa Everton akielekea kupanda kwenye basi waliloandaliwa.

 

Baada ya kuwasili walielekea hotelini kwa ajili ya mapumziko kisha baadaye watapata fursa ya kufanya mazoezi.

 

Everton wakiwa kwenye viunga vya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere

 

Everton wakipanda kwenye basi kuelekea hotelini kupumzika

 

Ni furaha ujio wa Everton Tanzania.

 

Hiki hapa kikosi kamili cha Everton waliowasili Tanzania leo:

Maarten Stekelenburg, Mateusz Hewelt, Chris Renshaw, Tom Davies, Phil Jagielka, Ashley Williams, Callum Connolly, Jonjoe Kenny, Michael Keane, Muhamed Besic, Leighton Baines, Morgan Schneiderlin, James McCarthy, Davy Klaassen, Gareth Barry, Idrissa Gana Gueye, Joe Williams, Kieran Dowell, Kevin Mirallas, Wayne Rooney, Aaron Lennon, Dominic Calvert-Lewin, Ademola Lookman, Matthew Pennington, Yannick Bolasie.

 

Wayne Rooney akijiselfisha na mashabiki kabla ya kuondoka Everton kuja Tanzania
Wayne Rooney akijiselfisha na mashabiki kabla ya kuondoka Everton kuja Tanzania

 

Everton walivyoondoka Uingereza

 

 

Leave A Reply