The House of Favourite Newspapers

BREAKING: FAMILIA YATOA SH. BIL 1 ATAKAYEFANIKISHA KUMPATA MO

FAMILIA  ya mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ aliyetekwa Alhamisi iliyopita na watu wasiojulikana, imetoa zawadi ya Sh. bilioni moja (1,000,000,000) kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwake.

Kauli hiyo imetolewa na familia hiyo kwenye mkutano na vyombo vya habari leo mchana katika ofisi za kampuni ya MeTL Group zilizopo katika jengo la Golden Jubilee Towers ghorofa ya 20 Mtaa wa Ohio, Posta,  jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa familia hiyo, Azim Dewji amesema, mwenye taarifa awasiliane na mwanafamilia Murtaza Dewji kwa namba 0755030014, 0717208478 na 0784783228  na email ya [email protected]

 

“Katika kuhakikisha mtoto wetu mpendwa anapatika mapema familia tunatangaza donge nono la Tsh bilioni 1 kwa yoyote atakayetoa taarifa muhimu zitakazopelekea kupatikana kwake na taarifa hizo zitakuwa ni siri kati ya mtoa taarifa na familia yetu.

 

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu na tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi zake kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuhakikisha kwamba mtoto wetu anapatikan, vyombo vya habari kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kulichukulia uzito jambo hili na kutoa taarifa kwa Umma, taasisi za kidini na zisizo za kidini na kila mmoja wenu kwa maombi ya kutufariji katika kipindi hiki kigumu familia inachopitia, amesema Azim.

 

Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Alhamisi Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam alipokuwa amekwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.

Global TV Online ilikuwa LIVE, Bofya HAPA

Comments are closed.