Breaking News: Felix Tshisekedi wa Upinzani Aongoza Kura za Urais Congo

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Ceni) imemtangaza mgombea wa upinzani, Felix Tshisekedi kuwa anaongoza katika kura za kiti cha Urais wa nchi hiyo baada ya kupata zaidi ya kura milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa kulingana na matokeo ya awali.

 

Mkuu wa Tume hiyo Corneille Nangaa, amesema mgombea huyo mpaka sasa anaongoza na kuwaaacha mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu aliyepata kura milioni 6.4 na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni.

 

Tshisekedi ambaye anatoka kwenye muungano wa kisiasa aliyekuwa mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation) Vital Kamerhe UNC ambapo walikuwa wamekubaliana kwamba Tshiskedi atagombea wadhifa wa rais naye Kamerhe awe waziri mkuu iwapo muungano wao utashinda urais, amekuwa mgombea wa kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi wa urais tangu DRC ilipojipatia uhuru.

Wagombea wakuu wa urais DR Congo

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume hiyo, matokeo kamili awali yalitarajiwa kutangazwa Jumapili lakini yakaahirishwa na sasa yanatarajiwa kutangazwa mnamo 15 Januari na rais mpya ataapishwa siku tatu baadaye. Matokeo hayo hata hivyo yanaweza kupingwa katika Mahakama ya Kikatiba.

 

Rais Joseph Kabila ambaye anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 18, alikuwa ameahidi kukabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi huo, jambo ambalo likitokea itakuwa mara ya kwanza tangu DRC kupata uhuru kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.

 

Walioruhusiwa kuwania urais DR Congo

 • Emmanuel Ramazani Shadary
 • Kikuni Masudi Seth
 • Mukona Kumbe Kumbe Pierre
 • Ngoy Ilunga Isidore
 • Makuta Joseph
 • Kabamba Noel
 • Mabaya
 • Kinkiey Mulumba
 • Freddy Matungulu
 • Felix Tshisekedi
 • Allain Shekomba
 • Radjabu Sombolabo
 • Kamerhe Vital
 • Fayulu Martin
 • Bomba
 • Gabriel Mokia
 • Basheke Sylvain
 • Charles Gamena
 • Mbemba Francis

 

Kulikuwa na wagombea 21 lakini watatu ndio wakuu:

 • Emmanuel Ramazani Shadary, Waziri wa zamani wa mambo ya ndani na mtiifu kwa Kabila, ambaye aliwekewa vikwazo na Muungano wa Ulaya kwa hatua zilizochuliwa upinzani wakati wa maandamano ya mwaka 2017.
 • Martin Fayulu, Mkurugenzi mkuu wa zamani wa mafuta ambaye ameahidi nchi yenye mafanikio lakini ambaye watu maskini wanahisi hawezi kuwatetea.
 • Felix Tshisekedi Tshilombo, Mtoto wa mwanasiasa mkongwe ambaye ameahidi kupambana na umaskini.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment