Breaking News: HATIMAYE Masele Ajisalimisha kwa Ndugai – Video

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (Pan-African Parliament – PAP) na Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Julius Masele ameitikia wito wa Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyemtaka kurejea nchini kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge jijini Dodoma.

Masele amewasili leo Jumatatu, Mei 20, 2019 Bungeni jijini Dodoma baada ya mvutano wa siku kadhaa na spika huyo ambaye aliagiza endapo asingerejea bungeni leo angetafutwa, kukamatwa na kutiwa pingu kisha kupelekwa kwa nguvu.

 

Akizungumza bungeni Dodoma Mei 16, mwaka huu, Ndugai alisema amemwandikia barua Masele areje nchini kutoka Afrika Kusini anakofanyia kazi za umakamu wa rais wa PAP, lakini mbunge huyo alidaiwa kukaidi wito wa spika na badala yake akasema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alimwelekza asiitikie wito huo, aendelee na kazi zake kama kawaida.

Ndugai alisema Masele ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hovyohovyo na anafanya mambo ambayo ni hatari kubwa, pia alitangaza kusitisha uwakilishi wa Masele kwenye PAP, hadi kamati za maadili za bunge  na CCM zitakapomalizana naye.

 

Spika ameitaka Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka Bunge kwenda kumuhoji Masele. Agizo hilo amelitoa leo Mei 20 wakati wabunge wakichangia mjadala wa Wizara ya Kilimo. “Nawaomba Kamati ya Maadili mwende sasa maana Mheshimiwa Masele ameishafika,” amesema Spika Ndugai.

TAZAMA MASELE AKIWA BUNGENI LEO


Toa comment