Breaking News: Jengo la Ghorofa Sita Laporomoka

RIPOTI nchini Kenya zinasema kuwa jengo la ghorofa sita limeanguka asubuhi ya leo katika eneo la Embakasi jijini Nairobi, huku watu kadhaa wakihofiwa kunaswa chini ya kifusi chake.

Shughuli za uokoaji zinaendelea na ripoti zinasema watu kadhaa wameokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

 

 

Updates

Watu watatu wakiwa na majeraha makubwawametolewa kutoka kwenye kifusi na kupelekwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta, jijini Nairobi, wakiwemo mama na mtoto.

 

Familia 46 zilikuwa wakuwa zikiishi kwenye jengo hilo. Polisi na kikosi cha Msalaba Mwekundu kutoka kaunti ya Nairobi wako kwenye eneo la tukio ambapo inasemekana wanapata wakati mgumu kudhibiti kundi kubwa la watu waliojitokeza kushuhudia mkasa huo.

Haijabainika ni kwa nini jengo hilo liliporomoka na watu wangapi wamenaswa ndani yake.  Mashuhuda wanadai  huenda kukawa na watu wengi wamekwama kwani jengo lenyewe liliporomoka mapema asubuhi na wakati huu shule zikiwa zimefungwa.

Wenyeji wanailaumu Idara ya Mipango ya Ujenzi nchini kwa kutohakikisha majengo yaliyojengwa ni salama kutumika.  Wanadai kuwa idara hiyo imezembea katika kukagua usalama wa majengo hasa jijini Nairobi na hivyo kuwaacha watu katika hatari.

 

Shughuli za kuwaokoa walionasa kwenye jumba hilo zinaendelea huku magari ya kubeba wagonjwa yakiwa yamefika kutoa msaada wa dharura. Mkuu wa Polisi, Philip Ndolo,  amesema kuwa wanafanya kila wawezalo kuwaokoa watu waliokwama.

Hili si jengo la kwanza kuporomoka. Mwezi Septemba mwaka huu jengo la ghorofa moja la shule eno la Dagoreti.  Nairobi,  liliporomoka na kuua wanafunzi saba huku wengine 64 wakijeruhiwa. Mwaka 2015, jengo jingine la ghorofa sita liliporomoka eneo la Huruma jijini Nairobi na kugharimu maisha ya watu kadhaa.

Wakati wa matukio hayo, serikali  ilianza ukaguzi wa majengo yote hasa ya makazi jijini Nairobi. Ripoti ya ukaguzi ilionyesha kuwa zaidi ya majengo 800 si salama na hivyo yalihitaji kubomolewa kwani hayakidhi viwango vya ubora.

 

Hata hivyo,  shughuli hiyo ilisimamishwa baadaye serikali ikidai haikuwa na fedha za kutosha kubomoa majengo hayo yote.
Toa comment