Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Mpambe wa Rais Kanali Mkeremi akiingia bungeni mjini Dodoma leo asubuhi akiwa na bahasha yenye jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge.Spika Job Ndugai akiinua bahasha kabla ya kusoma jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa bungeni na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge.Wakati hayo yakiendelea ndani ya bunge Mbunge wa Rwangwa Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili viwanja vya bunge akiwa peke yake bila shaka akiwa hana habari kwani usiri wa kupatikana na hatimaye kuwasilishwa jina la Waziri Mkuu Mteule ulikuwa mkubwa sana.
Bunge linaripuka na wabunge wanampongeza Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya jina lake kutangazwa na hatimaye kupigiwa kura na kupita kwa kishindo kwa kura 258 ama asilimia 73.5 ya idadi ya kura zilizopigwa.
Bunge linaripuka na wabunge wanampongeza Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya jina lake kutangazwa.
Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia nafasi hiyo, akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani aliyoonesha juu yake, anawashukuru pia wabunge kwa kumpa kura nyingi, na wapiga kura wake kwa kumchagua tena na kumuwezesha kufika hapo. Picha na Sultani Kipingo.
Waziri Mkuu Mteule wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ameshinda kwa kura za ndiyo 258 sawa na asilimia 73.5 ya kura zote zilizopigwa na wabunge leo, wakati kura za hapana zikiwa 91, sawa na asilimia 25.9.
Kassim Majaliwa alizaliwa Desemba 22, 1960 na ana umri wa miaka 54.
Ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
WASIFU WAKE:
Elimu | ||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||
Uzoefu | ||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||
Burudani | ||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Comments are closed.