Breaking News: Mbunge wa Newala Vijijini Afariki Gesti

MBUNGE  wa Newala Vijijini (CCM), Rashidi Ajali Ahkbar,  amefariki dunia leo Januari 15, 2020,  katika Gesti ya Mingoyo iliyopo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi na mwili wake unmechukuliwa na polisi na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi ya Sokoine kwa uchunguzi zaidi.

 

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mtwara, Selemani Sankwa, amesema taarifa za maziko zitatolewa baada ya makubaliano ya familia na Ofisi za Bunge.

 

CCM kimesema kinautambua mchango wa kiongozi huo enzi za uhai wake kwa kuwatumikia wananchi wa Newala Vijijini na kukijenga chama.


Loading...

Toa comment