The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: MO DEWJI APATIKANA!

Taarifa zilizotufikia alfajiri ya leo, Oktoba 20, 2018, zinasema kuwa Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo Dewji amepatikana na amerejea nyumbani kwake kuungana na familia yake akiwa salama. Kwa mujibu wa mtandao wa Makampuni ya Mohamed Enterprises ya MeTL Group, Mo amerejea nyumba ikiwa ni siku ya tisa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana Alhamis Oktoba 11 katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam.

 

Akitoa taarifa hizo kuptia mtandao wa Twitter unaomilikiwa na Kampuni yake ya Mohamed Enterprises Ltd, Mo ameandika: “Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji na , taarifa ambayo aliipost Saa 9:15 alfajiri, saa za Tanzania.

Aidha, Waziri wa Mazingira, Mhe. Januari Makamba, nae kupitia mtandao wake wa Twitter, amethibitisha kupatikana kwa Mo na kusema kuwa Mfanyabiashara huyo alitupwa maeneo ya Gymkhana huku akiwa na alama za kufungwa kamba mikononi.

 

Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri.,” ameandika Makamba.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  amethibitisha  kupatikana kwa Mo Dewji.

Kipande cha video RPC Mambosasa akithibitisha kupatikana kwa Mo Dewji alfajiri ya leo.

Comments are closed.