Breaking News: Moto Wateketeza Maduka Tegeta-Nyuki Dar

MADUKA saba katika soko la Tegeta-Nyuki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam yameteketea kwa moto leo asubuhi Februari 18, 2020.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Musa Taibu,  amesema moto huo ulianza majira ya saa sita usiku na bado chanzo chake hakijafahamika.

 

“Ni kweli moto umeshika sehemu ya maduka na si soko lote, vibanda saba vimeteketea. Baada ya kupata taarifa polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifanikiwa kuuzima,” amesema.

Amesema uchunguzi umeanza kubaini chanzo na hasara iliyosababishwa na moto huo.

“Bado chanzo hakijafahamika, tunafanya uchunguzi kubaini. Hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha,” amesema.

 

Juma Athuman,  mfanyabiashara wa eneo hilo amesema kuwa alipigiwa simu saa saba usiku kuwa maduka yao yanaungua na moto;

 

“Baada ya kupata taarifa ile nilitamani kuruka kutoka Mabibo mpaka Tegeta lakini sikuwa na uwezo huo, nikampigia jirani yangu mwenye usafiri ndipo akanileta huku, lakini sikuwa na la kufanya kwani tayari maduka yalikuwa yameshaungua,” alisema.


Loading...

Toa comment