The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE AFARIKI DUNIA

IKIWA ni siku tisa tangu kituo cha Utangazaji cha Clouds Media kupata pigo kwa kuondokewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, chombo hicho cha habari kimepata pigo jingine tena leo kwa kuondokewa na mtangazaji wake, Ephraim Kibonde, kilichotokea alfajiri ya leo, Alhamisi, Machi 7, 2019.

 

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Clouds Media wameandika:

“Tukiwa bado na majeraha mabichi ya msiba wa mMkurugenzi wetu wa Vipindi na Uzalishaji #Ruge Mutahaba, kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Mtangazaji wetu  Ephraim Kibonde kilichotokea alfajiri ya leo (Machi 7, 2019).

“Tunamtukuza Mungu kwa maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele. Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.

 

Kupitia Twitter pia wameandika:

“Tunamtukuza Mungu kwa Maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele. Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.

 

Imeelezwa kuwa, Kibonde amefariki akiwa Mwanza na alianza kusumbuliwa na presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Ruge.

 

Julai 10, 2018, Kibonde alipata pigo la kuondokewa na mkewe, Sara Kibonde,  ambaye alifariki dunia usiku huo wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Hindu Mandal.

 

Uongozi na wafanyakazi wa makampuni ya Global Group unatoa pole kwa wafanyakazi wa Clouds Media kutokana na msiba huu.  Unamwomba  Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu mnachopitia. Poleni sana ndugu zetu.

Comments are closed.