Mtoto Warda Mohammed Apatikana Chamazi Dar
Mtoto Warda Mohammed (15) aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu iliyopo Kibaha mkoani Pwani aliyepotea tangu Aprili 19, 2023, amepatikana.
Usiku wa kuamkia Oktoba 28, 2023, GLOBAL TV imepokea simu kuwa Warda ameonekana Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar.
GLOBAL TV imefunga safari na kwenda kumshuhudia Warda na kumtambua kuwa kweli ni yeye.
Kwa mkasa mzima, usikose kufuatilia kipindi cha Mapito Jumapili hii ambapo simulizi nzima itasikika mwanzo hadi mwisho.