The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE – Video

Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 30, 2018, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22 ikilinganisha na mwaka 2016.

 

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,  Dk Charles Msonde ameeleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu wakiwemo wanafunzi 136 waliofanya mtihani wa kujitegemea (Private Candidate) na 129 waliofanya mtihani wa shule (School Candidate).

“Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22,” alisema Msonde.

Amemtaja mwanafunzi aliyeongoza kitaifa kuwa ni Ferson Mdee kutoka Shule ya Sekondari Marian Boys.

KUANGALIA MATOKEO YOTE BONYEZA LINK HAPA CHINI

 

Link 1: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2017

Link 1: MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2017

Link 2: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2017

 

MSIKIE MSONDE AKITANGAZA MATOKEO HAYO

Comments are closed.