The House of Favourite Newspapers

BreakingNews: CCM Yaapa Kuwashughulikia Kikamilifu Makada Waliotajwa Ripoti ya Mchanga wa Madini (+VIDEO)

0

Chama cha Mapinduzi (CCM), kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, kimesema kinasubiri majibu ya uchunguzi wa tuhuma zilizoelekezwa kwa makada wakongwe wa chama hicho, kuhusu kuhusika kwao katika kusafirisha mchanga wa madini kwenda nje ya nchi na kusaini mikataba mibovu ya madini.

 

Polepole amesema chama chao kinaongozwa kwa kanuni na sheria kwa hiyo ipo wazi kwamba hakitawavumilia wote waliotajwa kwenye sakata la kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha.
Aliongeza kwamba japokuwa mambo yote yametokea kwenye serikali ya CCm, ni jambo la kujivunia kuona kwamba CCm yenyewe ndiyo iliyochukua jukumu la kurekebisha makosa yaliyotokea miaka ya nyuma, na itahakikisha Tanzania mpya inapatikana.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Polepole alisema chama kinampongeza mwenyekiti wao, rais Magufuli na kinamuunga mkono kwa hatua ya uzalendo aliyoichukua ya kuhakikisha analinda rasilimali za taifa, akaongeza kwamba kamwe hakuna kurudi nyuma.

 

Leave A Reply