The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Polisi Dar Yakamata Silaha Nzito – Video

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata silaha mbalimbali zikiwemo bunduki kubwa, bastola na vifaa vingine vya uhalifu pamoja na watuhumiwa mbalimbali wa uhalifu waliokuwa wakijiandaa kutekeleleza matukio hayo.

 

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasaamesema jeshi hilo limekamata silaha aina ya AK 47 na watuhumiwa wawili nyumbani kwa mzee Said Omary (62) baada ya kupata taarifa kuwa kuna wahalifu wanataka kufanya tukio la wizi wa kutumia silaha.

 

“Tulipowakamata wakasema silaha hiyo waliiokota kwenye vyuma chakavu, lakini tulipowahoji walitoa taarifa wapi wakasema hawakutoa taarifa badala yake walikuwa wakitafuta soko ili kuiuza silaha hiyo,” alisema Mambosasa.

 

Aidha Polisi imewakamata watuhumiwa 2 wa wizi wa magari ambao baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na radio call, kadi 10 za benki mbalimbali, leseni mbili za udereva, master keys 15 ambapo baada ya kuhojiwa walikiri kutekeleza matukio mbalimbali ua uhalifu huku wakionesha magari mawili na pikipiki moja vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi.

 

Mbali na matukio hayo, polisi pia imekamata watuhumiwa sita walikamatwa wakiwa na vielezo mbalimbali zikiwemo telebisheni 8, sabufa na vingine.

 

MSIKILIZE KAMANDA MAMBOSASA AKIFUNGUKA

Comments are closed.