The House of Favourite Newspapers

Polisi Yawakamata Waliovamia Ofisi za Mawakili wa Manji -Video

0
Ofisi za Prime Attorneys zilizovamiwa.

JESHI la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatia mbaroni watu watano wanaodaiwa kuvamia, kuvunja na kuiba pesa kwenye ofisi za Prime Attorneys anazofanyia kazi wakili anayemtetea  Yusuf Manji, Hudson Ndusyepo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa wamekamatwa kufuatia oparesheni kali.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari.

   

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar mnamo Septemba 12, 2017 lilipokea taarifa za kuvamiwa kwa ofisi za Prime Attorneys ambapo watuhumiwa walivunja na kuiba pesa taslim Tsh. Milioni 3.7, kompyuta, laptop mbili, nyaraka za ofisi na za wateja wao.

Silaha na bomu la kurushwa kwa mkono zilizokamatwa.

Baada ya msako huo watuhumiwa walikamatwa na walipohojiwa, wote wamekiri kuhusika na tukio hilo huku wakitaja matukio mengine waliyohusika kupora. Pia wameonyesha pesa walizopora kwenye tukio hilo.

Watuhumiwa hao ni; Said Idrisa Saleh (47), mkazi wa Mbezi Luis, Musatapha Ibrahim Said (35), mkazi wa Magomeni Mwembechai, Somfi Nguza Somfi (52), mkazi wa Magomeni Mapipa, Imani Mbago Mhina (36), mkazi wa Kimara Mwisho na Hussein Hajji Suleiman (45), mkazi wa Kigogo Mbuyuni.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema jeshi lake linaendelea na upelelezi kubaini watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.

..Mambosasa akionyesha bomu la kurushwa kwa mkono lililokamatwa katika oparesheni hiyo.

Ofisi za kampuni hiyo zipo jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam jirani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala.

 

MAJAMBAZI WATATU WAUWAWA, WAWILI WAKAMATWA NA KUPATIKANA SILAHA AINA YA UZIGUN, RIFFLE NA BASTOLA AINA YA BROWNING NA JUMLA YA RISASI 170

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 15/09/2017 majira ya saa kumi na moja na dakika ishirini jioni huko maeneo ya Vingunguti-BECCO mkoa wa kipolisi Ilala, askari wa kikosi cha kupambana na ujambazi walipata taarifa kuwa kuna majambazi wanaenda kufanya tukio la kiuhalifu kwenye moja ya maghala eneo la TAZARA.

Askari waliweka mtego na kulisimamisha gari aina ya Toyota Mark II rangi ya blue namba zake za usajili hazikufahamika, baada ya kugundua ni askari wanawafuatilia majambazi hao walianza kuwashambulia askari kwa risasi ndipo askari wakajibu mashambulizi na kuwajeruhi majambazi watatu.

Majambazi hao wamegunduliwa kuwa ni wahalifu sugu miongoni mwao anajulikana kwa jina la SHAFI huyu alitoka gerezani siku za hivi karibuni baada ya kuachiwa kwa rufaa ambako alikuwa akitumikia kifungo cha miaka thelathini jela kwa kosa la Unyang’aji wa Kutumia Silaha. Mtuhumiwa mwingine alitambulika kwa jina la BABU JAFFARI ana matukio mbalimbali ya Unyang’anyi wa kutumia Silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji la DSM ambapo kwa mara ya mwisho alikuwa akiripoti kituo cha Polisi Chang’ombe. Jambazi wa tatu anaitwa MBEGU @ MALON huyu ndiye mtafutaji wa kazi za kwenda kupora likiwemo tukio hilo la TAZARA

Eneo la tukio pamekutwa Bastola moja aina ya BROWNING risasi tatu moja ikiwa chemba tayari kwa kutoka, maganda matatu ya risasi zilizofyatuliwa kutoka katika Bastola ya majambazi. Majambazi hao walifariki wakati wanapelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu baada ya kuvuja damu nyingi, msako mkali unaendelea kumsaka jambazi aliyetoroka na gari waliotumia majambazi hao.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 16/09/2017 majira ya saa Kumi na moja na dakika hamsini jioni huko maeneo ya makaburi ya Wangazija, Upanga walikamatwa RAHMA ALMAS @ BABY miaka 37 mkazi wa Temeke mtaa wa Mkuranga B na MOHAMED MAGANGA miaka 61 mkazi wa Pugu mfanya usafi na ni mlinzi kwenye makaburi hayo ya Wangazija eneo hilo wakiwa na Bunduki mbili aina ya UZIGUN na Riffle, bomu la kurusha kwa mkono, risasi 162 za silaha aina ya Uzigun, na risasi tano za silaha ya Riffle.

Baada ya mahojiano mtuhumiwa RAHMA ALMAS @ BABY alikiri kuhifadhi silaha hizo zilizotumika katika matukio mbalimbali ya kiuhalifu jijini DSM ikiwemo mauaji ya WAYNE DERRICK LOTTER mkurugenzi wa PALM CONSERVATION FOUNDATION miaka 52 raia wa Afrika ya Kusini.

Mtuhumiwa huyo aliwaelekeza askari kuwa silaha hizo amezificha katika makaburi hayo, ndipo askari walifika eneo la tukio na mtuhumiwa huyo na walizikuta silaha hizo mbili moja ikiwa ni aina yaUzigun nyingine ni bunduki aina ya Riffle ambaye imekatwa mtutu na kitako zake na namba zikiwa zimefutwa zote zikiwa zimefukiwa kwenye shimo.

Mtuhumiwa wa pili MOHAMED MAGANGA ambaye ni mlinzi na mfanya usafi wa makaburi hayo ambaye alisaidia kuchimba shimo na kuzilinda silaha hizo, alikiri silaha hizo zililetwa na mtuhumiwa RAHMA ALMAS na mlinzi huyo hakutoa taarifa mpaka alipokamatwa. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

WATUHUMIWA WATANO WAKAMATWA KESI YA UVUNJAJI WA OFISI YA MAWAKILI ITWAYO PRIME ATTORNERYS

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 12/09/2017 majira ya 01:45 hrs lilipokea taarifa ya kuvunjwa kwa ofisi ya mawakili iitwayo Prime Attorneys ambapo wahalifu hao walifanikiwa kuiba kasiki iliyokuwa na pesa Tsh 3,700,000/=, laptop mbili pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi na za wateja.

Katika mwendelezo wa tukio hilo watuhumiwa watano wamekamatwa baada ya oparesheni kali ya kuwatafuta waliovunja ofisi hiyo ya PRIME ATTORNERYS. Watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo mbalimbali ya jiji la DSM. Watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na;

1. SAID IDRISA SALEHE miaka 47 mkazi wa Mbezi Luis,

2. MUSTAPHA IBRAHIM SAID miaka 35 Mkazi wa Magomeni Mwembechai

3. SOMFI ULIZA SOMFI miaka 52 mkazi Magomeni Mapipa,

4. IMAN MBAGO MHINA miaka 36 mkazi wa Kimara Mwisho

5. HUSSEIN HAJI SULEIMAN miaka 45 mkazi wa Kigogo Mbuyuni

Baada ya mahojiano watuhumiwa hao walikiri kushiriki tukio hilo na kuonyesha Kasiki la fedha pamoja na mitungi mitatu ya gesi iliyotumika kukatia Kasiki hilo, ambapo baada ya kuiba walienda Magomeni Mapipa mtaa wa Dosi kwa mtuhumiwa aitwaye SOMFI ULIZA SOMFI, baada ya kulifungua na kukuta hakuna fedha walilichukua na kulitekeleza eneo la Kigogo daraja la Madaba.

Upelelezi unaendelea ili kuwabaini watumiwa wengine walioshiriki tukio hilo.

POLISI KANDA MAALUM DSM KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUANZIA TAREHE 15.09.2017 HADI TAREHE 18.09.2017 KIMEFANIKIWA KUKUSANYA TSH 424,620,000 /=KWA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani kinaendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 15.09.2017 hadi tarehe 18.09.2017 kama ifuatavyo:-

1. Idadi ya magari yaliyokamatwa – 13,784
2. Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa – 392
3. Daladala zilizokamatwa -5,387
4. Magari mengine (binafsi na malori) -8,397
5. Bodaboda waliofikishwa Mahakamani
kwa makosa ya kutovaa helmet na kupakia mishikaki -22

Jumla ya Makosa yaliyokamatwa – 14,176

6. Fedha za Tozo zilizopatikana – 424,620,000 /=

L.B.MAMBOSASA – SACP
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply