Breaking News: Prince Charles, Agunduliwa na Virusi vya Corona, Malkia Yu Salama

MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza,  na mrithi wa kwanza katika msululu wa taji la ufalme la nchi hiyo, amegundulika kuwa na virusi vya Corona na sasa amejitenga peke yake huko Scotland.

 

Katika taarifa iliyotolewa na makao makuu ya kifalme nchini humo, Malkia yuko salama.

 

“Prince of Wales amegundulika kuwa na virusi vya Corona.  Pamoja na kuonyesha dalili kadhaa za ugonjwa huo, yuko katika hali njema na amekuwa akifanya kazi zake akiwa nyumbani mnamo siku chache zilizopita.” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

 

“Haiwezekani kutambua mahali alipovipata virusi hivyo kutokana na kazi nyingi alizozifanya katika jamii katika wiki za karibuni.”

Toa comment