Breaking News: Profesa Benno Ndulu Afariki Dunia

 

ALIYEWAHI kuwa Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu (71), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Februari 22, 2021 katika hospitali ya Hubert Kairuki Memorial University alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

 

 

Katibu muhtasi wake, Msafiri Nampesya, ameithibitisha kutokea kwa kifo hicho.

 

 

Profesa Ndulu alikuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, kuanzia 2008 hadi 2018 na pia aliwahi kuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliwahi kufanya kazi Benki ya Dunia.

 

 


Toa comment