The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Rais Magufuli Amtumbua Mkurugenzi Butiama

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleimani Jafo ametangaza kuwa, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Butiama mkoani Mara, Solomoni Ngiliule kuanzia leo kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza maamuzi hayo leo zikiwa zimepita siku tatu toka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotoa maagizo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

 

Waziri Mkuu aliagiza kiongozi huyo kuchunguzwa kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo huku fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu maalumu, sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazikujulikani zimetumikaje.

 

TBC: MIGOGORO YA ARDHI ILIVYOKITHIRI MAKETE

Comments are closed.