BREAKING NEWS: RAIS MORSI AFARIKI DUNIA GHAFLA MAHAKAMANI

ALIYEKUWA rais wa Misri, Mohammed Morsi, akatimuliwa madarakani na jeshi mnamo 2013, ameaga dunia ghafla akiwa mahakamani, televisheni ya taifa imesema.

 

Mahakama nchini Misri ilibatilisha hukumu ya kifo mnamo 2016 dhidi ya rais huyo aliyepinduliwa.

 

Morsi alikumiwa kifo baada ya kulaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 nchini humo.

 

Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa katika mapinduzi ya jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

 

Morsi alishahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi.

 

Mwanasiasa huyo alizaliwa Agosti 8, 1951 na amefariki Juni 19, 2019 akiwa ni rais wa tano wa Misri, nafasi aliyoishika tangu Juni 30, 2012 hadi Julai 3, 2013 alipong’olewa na Jenerali Abdl Fattah el-Sisi katika mapinduzi yaliyofuatia maandamani nchini humo.

 

Tutakujuza zaidi kuhusu taarifa hii kadri tunavyoendelea kupokea maelezo.

 

 


Loading...

Toa comment