The House of Favourite Newspapers
gunners X

Breaking News: Rais Mstaafu Moi Afariki Dunia

0

RAIS Mstaafu wa Kenya, Daniel arap Moi, amefariki dunia akiwa na miaka 95, rais Uhuru Kenyatta athibitisha.

“Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha kiongozi mkubwa Afrika, Daniel Toroitich arap Moi, rais wa pili wa Kenya. Raisi mstaafu amefariki katika Hospitali ya Nairobi mapema asubuhi ya leo Februari 4 akiwa na familia yake.

 

Msemaji wa  Moi, Lee Njiru,  pia amesema taarifa hizo zilisambaa kabla ya Ikulu kutoa tamko.

 

“Alikuwa Nairobi Hospital ambapo alilazwa tarehe 10 mwezi wa kumi mwaka uliopita, hiyo ni zaidi ya miezi mitatu,” Njiru amesema.

 

Kwa mujibu wa Njiru mipango yote ya mazishi ipo chini ya jeshi la Kenya kwa kuwa Moi alikuwa amiri jeshi mstaafu wa nchi hiyo. Runinga ya taifa ya Kenya (KBC), pamoja na vyombo binafsi vya Capital FM, Citizen TV na NTV vimeripoti taarifa hiyo ya msiba asubuhi ya leo Jumanne, Februari 4.

 

Moi alizaliwa Septemba 2, 1924 na alitawala Kenya kwa miaka 24 kutoka 1978 mpaka 2002.

 

Tangazo kutoka Ikulu limesema kuwa  Moi, hata baada ya kuondoka madarakani aliendelea kulitumikia taifa la Kenya na Afrika kwa kuwafundisha viongozi wa Kenya na nje ya Kenya, akiendelea kushiriki kwenye maendeleo ya miradi mbalimbali na kazi za misaada akihubiri amani, upendo na umoja barani Afrika na duniani.

 

Leave A Reply