Breaking News: Mugabe Afariki Dunia

RAIS  mstaafu wa Zimbabwe, Robert Mugabe,  amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Rais Mugabe alikuwa nchini Singapore akipatiwa matibabu kwa muda mrefu. Alikuwa rais wa nchi hiyo kutoka mwaka 1987 mpaka 2017, alipong’olewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.

Mugabe aliyezaliwa February 21, 1924, alitawala nchi hiyo kwa kuudhoofisha upinzani kupitia mabadiliko mbalimbali aliyoyafanya katika katiba ya nchi hiyo.

Habari za kifo chake zilitangazwa kwa watu wa nchi hiyo na kwa jumuia ya kimataifa na Rais Emerson Mnangawa kwa ujumbe uliopo chini.

 

Loading...

Toa comment