The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Rostam Aziz Atinga Ikulu, Akutana na Rais Magufuli – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara Rostam Aziz Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumanne Novemba 13, 2018.

Akizungumza wakati akiagana na Rais Magufuli, Rostam amesema; “Nimekuja kumuona Rais wangu na mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi (CCM). Nimekuja kumpongeza kwa kazi nzuri anazozifanya, namtakia kila la kheri. 

“Kama mfanyabiashara, naona kinachofanyika sasa hivi ni kutengeneza msingi ya uchumi, ambao utakuwa kwa uhakika zaidi. Watu waweze kufanya biashara zao kwa uhuru na haki, hivyo ndivyo uchumi utakavyoendelea kukua, kuliko huko nyuma,” alisema Rostam.

Rostam ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Igunga kwa tiketi ya CCM anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1, (kulingana na taarifa za Jarida la Forbes za Julai 2015)

 

Akram Aziz Abdul Rasool ambaye ni mdogo wa Rostam Aziz anakabiliwa na mashtaka 75 katika kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Kisutu, Dar, ikiwemo ya kudiwa kukutwa na meno ya tembo, silaha na risasi.

BREAKING: Rostam Aziz Atinga kwa JPM Leo

Comments are closed.