Breaking News: Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa -Dar

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa.

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, jana Septemba 12, maeneo ya Kivule Chanika lilifanikiwa kumuua jambazi sugu aitwae Anae Rashid Kapela aliyekuwa akitafutwa na jeshi hilo kwa muda mrefu akituhumiwa kushiriki matukio mbalimbali ya ujambazi likiwemo la mauaji ya polisi wanane wilayani Kibiti.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro  Mambosasa alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar.

“Baada ya kupewa taarifa na wasamalia wema, Jeshi hilo lilifika na kuizingira nyumba alimokuwa lakini alifanikiwa kutoka na kutaka akitoroka. Polisi walipomsimamisha alikimbia ndipo wakampiga risasi ya goti na kuanguka.

“Alipohojiwa alitaja mlolongo wa matukio mbalimbali ya uhalifu aliyoshiriki kuyafanya likiwemo hilo la kuwaua Askari Polisi wakiwa lindoni pale CRDB Mbande, uvamizi wa benki ya NMB Mkuranga, Access Bank Mbagala na mauaji ya askari wanane na kupora silaha zao Kibiti Mkuranga, yeye alikuwa kiongozi wao,” alisema Mambosasa.

“Jambazi huyo aliwataja pia wahalifu wakuu aliokuwa akitenda nao kazi, ndipo polisi wakamkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu, lakini kabla ya kufika hospitali alifariki akiwa njiani kutokana na kuvuja damu nyingi,” aliongeza Mambosasa.

SHUHUDIA VIDEO YA TUKIO HILO


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment