The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Watu Saba Wafariki kwa Ajali Wilayani Kiteto Mkoani Manyara

0

 

Watu sita ambao ni watumishi wa serikali ya wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Idara ya afya na elimu wamefariki dunia kwa ajali baada ya gari waliyokuwa wamepanda kugongana na gari lingine aina ya Toyota Prado katika eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo wilayani Kiteto mkoani Manyara.

 

Katika ajali hiyo watu wengine watano wamejeruhiwa na wamehamishwa kwenda hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga akiwa Hospitali ya Kiteto amethibitika kutokea ajali hiyo.

Batenga amesema ajali hiyo imehusisha gari la wagonjwa, Ambulance ya Kituo cha Afya Sunya lililokuwa limeleta mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa ajili ya matibabu na wakati likirudi likiwa limebeba watumishi kurejea eneo la kazi Sunya liligongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Prado likitokea Barabara ya Kilindi-Tanga kuelekea Kiteto.

 

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kiteto, Pascal Mbota, amesema amepokea miili ya watu wawili waliopoteza maisha na majeruhi kumi na moja.

 

Kati ya majeruhi hao wanne wamefariki katika harakati za kuwaokoa, watano wamesafirishwa kwenda Hospitali ya Dodoma kwa matibabu na wawili wanaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Kiteto.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, RPC George Katabazi amethibitisha ajali hiyo akisema majina ya waliopoteza maisha na waliopelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na wanaoendelea na matibabu Hospitali ya Kiteto yatatolewa leo.

Leave A Reply