The House of Favourite Newspapers

Waziri Kigwangalla Ahamishiwa Dar

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyepata ajali ya gari leo mkoani Manyara anahamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi akitokea mkoani Arusha.

 

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema licha ya waziri huyo kuendelea vizuri, anahitaji matibabu zaidi.

 

Amesema ndege itakayomchukua waziri huyo ipo Arusha na kwamba ataambatana na watu kadhaa.

Kuhusu mazishi ya Temba, amesema  yatafanyika kesho saa saba mchana nyumbani kwao  Masama wilayani Hai mkoani Kilimanjaro

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangalla.

 Waziri Kigwangalla Ahamishiwa Hospitali ya Selian, Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamis Kigwangalla amehamishiwa katika Hospitali ya ya Rufaa ya Selian, jijini Arusha kwa helkopta kutoka katika kituo cha afya cha Magugu, Manyara alipopelekwa baada ya kupata ajali.

Muonekano wa Hospitali ya ya Rufaa ya Selian jijini Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangalla wakati akitolewa kwanye helkopta nje ya Hoteli ya Kitalii ya Mount Meru jijini Arusha.

Comments are closed.