BREAKING NEWS: WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AJIUZULU – Video

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Theresa May,  ametangaza kujiuzulu wadhifa huo leo, Ijumaa, Mei 24, 2019, kutokana na shinikizo la chama chake cha Conservative. May pia ametangaza kuwa atajiuzulu kukiongoza chama chake ifikapo Juni 7, 2019 na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

 

Katika taarifa iliyojaa hisia aliyoitoa leo Downing Street, Bi May amesema amefanya “kila awezalo” kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016. Ni jambo linalosalia kuwa “na majuto mengi” kwamba ameshindwa kutimiza Brexit – Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza —  lakini waziri mkuu mpya ndiyo suluhu ” kwa manufaa ya taifa”.

May ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wa pili wa kike kuanzia Julai 13, 2016.  Amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa Chama cha Conservative na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayofuata baada ya hatua hiyo.

Katika taarifa yake ya kujiuzulu, May amewataka wananchi wenzake kuendeleza muungano uliopo bila kujali tofauti zao za rangi za ngozi.

Sauti yake ilitetereka na alikuwa mwingi wa hisia alipomaliza hotuba yake akisema: “Nitaondoka katika wadhifa huu hivi karibuni lakini imekuwa heshima kubwa maishani mwangu kuhudumu kama waziri mkuu mwanamke wa pili, na bila shaka si wa mwisho.

 

“Nachukua hatua hii bila ya kuwa na nia mbaya, bali natoa shukurani za dhati na kubwa kutokana na kupata fursa ya kuitumikia nchi ninayoipenda,” amesema May.

 

Wanaotajwa kuchukua wadhifa wa May ni hawa;
Matt Hancock
Esther McVey
Sajid Javid
Boris Johnson
Amber Rudd
Rory Stewart
Andrea Leadsom
Jeremy Hunt
Liz Truss

TAZAMA ALIVYOJIUZULU

Loading...

Toa comment