The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Wema Afutiwa Mashtaka, Aachiwa Huru

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi, Julai 4, 2019, imemfutia shtaka la kusambaza video isiyo na maadili mwigizaji maarufu wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, chini ya Kifungu 225(5) cha Sheria ya Uendeshaji Makosa ya Jinai na KUMUACHIA HURU.

 

Wakili wake, Albert Msando, amethibitisha na kuandika: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemfutia  @wemasepetu shtaka la kusambaza video isiyo na maadili chini ya Kifungu 225(5) cha Sheria ya Uendeshaji Makosa ya Jinai na KUMUACHIA HURU. @wemasepetu alishtakiwa kwa kosa hilo Mwezi Novemba, 2018. 

Adhabu kwa kosa hilo ni faini isiyopungua Shilingi Milioni Thelathini au Kifungo kisichopungua miaka 10 jela au vyote. 

WITHOUT PREJUDICE: KILA MMOJA ANAPASWA KUJIFUNZA MATUMIZI BORA YA MITANDAO YA KIJAMII. 
Kutukana, kutumia lugha chafu, kudhalilisha, kukashifu, KUSAMBAZA picha zisizoruhusiwa nk ni makosa na ADHABU zake ni kali sana. Usichukulie poa. #TheDon.

Comments are closed.